Saturday, March 7, 2020

Mambo 6 ambayo ni siri ya mwanamke na sio rahisi kukwambia

1. Idadi ya wapenzi wake wa zamani

Wanaume wengi hupenda kujua wao ni wangapi kuwa na mwanamke Fulani. Lakini mwanamke kamwe hawezi akakwambia wewe ni wa ngapi. Kumuuliza jambo hili kunamkera sana mwanamke na ndio maana mara nyingi hawezi akakwambia ukweli.

2. Anakulinganisha na mpenzi wa zamani

Mwanamke mara nyingi anakulinganisha na mpenzi wake wa zamani japokuwa hawezi kukwambia waziwazi. Wakati mwingine tabia hii huwafanya wanawake kuwatamani wapenzi wa zamani na hata kurudiana nao endapo watakosa mtu aliye bora kuliko mpenzi wake wa zamani.
>

3. Kasoro zako

Mwanamke kamwe hawezi kukwambia kasoro zako. Wanawake wanajua kumfichiaa mpenzi wao mambo wasiyotaka yajulikane kwa wengine na kwa mpenzi wake. Wanajua njia za kiujanja za kutumia ili kufichua siri zako zote. Mwanamke hawezi kukwambia kasoro zako kwa kuogopa kukuumiza.

4. Mapungufu yake

Mwanamke hawezi kukwambia mapungufu yake labda kwa kuhofia kusheshwa thamani. Wanawake ni wasiri sana kwa mapungufu yao. Wanajua vyema hofu zinazomuandamana, vitu vinavyowakosesha usingizi na mambo yanayowalemea maishani japo sio rahisi kuonyesha. Kwa nje anaweza akaonekana yuko vizuri na hana tatizo kumbe ndani ana matatizo au mapungufu. Anaweza kufanya yote kufunika upungufu wake!

5. Huwa unampagawisha mpaka anakosa la kusema

Hili halisemi kabisa mwanawake kwa sababu anaona haya kutumia maneno ya wazi kueleza raha unayompa. Maneno ya kuzuzua ni himaya ya wanaume, lakini wakati mwingine wapo wasioweza kuficha.

6. Haumridhishi katika tendo la ndoa

Wanawake wengi hawapendi kusema kama hawaridhiki Kwenye tendo la ndoa. Wanawake wanahitaji kuandaliwa vilivyo kwa dakika 10, 20 ama nusu saa. Mara nyingine wanaume huwahi kabla mwanamke hajawa tayari na hivyo kushindwa kuridhika lakini hawezi kusema

Thursday, March 5, 2020

Zijue Silaha Tano Muhimu za Kulinda Maahusiano Yako..!!!


Maisha ya mapenzi ya kweli ni yale yaliyo na furaha pande zote mbili na kwamba kila mmoja anaridhika na mwenzi wake kwa hali na mali.

Mapenzi kama yanavyosemwa na watu ni sanaa kama sanaa zingine zilivyo. Kama ni mchezo, basi una sheria zake. Leo nakuonyesha mbinu ambazo ukizingatia ndoa yako haitokuwa na matatani.

Ni maoni tofauti tofauti kutoka kwa wadau pamoja na wazoefu wa masuala haya ya mahusiano.
Upendo

Kila mwanaume anataka kujisikia anapendwa. Anataka kuona kuwa mwenza wake anampenda kiuhalisia na anamjali wakati wowote.

Heshima

Hata pale anapokuwa hayupo, anataka mwenzake wake awe nyuma yake, kumuongelea na kumheshimu.

Kukubalika

Kila mwanaume anataka kujisikia mwenza wake anamkubali na kumthamini kwa mambo mbalimbali kama vile penzi lake, muda, jitihada, anavyojituma na kila anachokifanya kwa mwenza wake.

Yeye ni bora zaidi

Anataka mwenza wake kujisikia kuwa yeye ni bora zaidi. Kila mwanaume anataka ajisikie kuwa yeye ni mwanaume bora zaidi kuliko wote aliowahi kuwa nao, na wengine wanataka kujisikia kuwa ni mwanaume pekee ambaye umewahi kuwa naye hata kama anajua si kweli.

Uaminifu

Mwanaume anahitaji mwenza wake awe mwaminifu. Uaminifu husaidia kujenga mapenzi zaidi, kila kitu kwa mwanaume na kadiri mwenzake anavyokuwa mwaminifu, ndivyo hawezi kuwa na wivu kwani anakuwa ameshajiaminisha.

Ukweli

Kila mwanaume anahitaji kujua kuwa anaweza kumwamini mwenza wake na kwamba naye anamwamini, ukiwa mkweli ni rahisi mume kukujengea imani, kuwa mkweli kwa kila jambo.

Nimekuwa Mtumwa wa Wanawake


Nimeficha ficha haya mambo ila najiona kabisa naangamia hivyo ni bora leo niombe ushauri maana hapa pana watu wazima, wanasaikolojia na viongozi wa dini.

Mkasa wangu ni wa hakika na bado nipo katika mateso hata sasa.

Wakati nipo balehe nilikutana na wasichana mbali mbali waliouteka moyo wangu na nikawaeleza hisia zangu, kwa bahati mbaya nilijibiwa karaha na kutoswa sababu ya maisha yangu ya dhiki.

Hali ilikwenda hivyo kwa muda mrefu mpaka moyo wangu ukajenga chuki na wanawake, niliwaona hawana usawa na sio wa kuwa nao karibu.

Katika utafutaji wangu wa maisha ghafla mambo yakabadilika na nikawa nina pesa na kuishi vizuri na nikaanza kujenga nyumba na pia nikawa na miradi pamoja na gari ya kutembelea.

Ni hapo ndipo wasichana wakaanza kuwa karibu na mimi na kunihitaji kimapenzi, na mimi nilishajenga chuki moyoni na nikapanga kuwakomoa, nikajikuta natembea na wanawake wengi tofauti kuanzia wanafunzi, walimu, wasichana tu wa mtaani, machangudoa na wapenzi wa watu.

Nikajikuta dhaifu mbele ya wanawake yaani siwezi kulala hata siku moja peke yangu bila mwanamke na pia mda mwingine nilifanya mapenzi na wasichana wawili tofauti kwa siku moja, haswa kama huyo wa pili aliyenitafuta ni mzuri sana.

Haya mambo sipangi bali najikuta tu inatokea na kila nikimaliza najuta na kusema ndio mara ya mwisho ila punde tu naingia katika vishawishi tena, nilioa mke safi kabisa ili niepuke hali hii ila tuliachana baada ya kunifumania mara kadhaa.


Sasa nina mke mwengine na safari hii nimeoa mke wa ndoto yangu mtoto mzuri sana shombe shombe kiasi kwamba marafiki wanasema kweli mwamba umepata kifaa.

Ila bado ninajikuta natembea na rafiki zake pia wasichana wa mtandaoni kama vile Jf, Badoo, Fb nk na pia nimekuwa maarufu madanguro mengi sana mpaka naona noma.

Mara kadhaa nasafirisha mademu wakali toka mikoa tofauti na kunifuata mimi, sihongi sana na wala sijatetereka ki uchumi na wala sijaathirika ila tu najiuliza nini kipo nyuma ya nguvu hii inayonishinda kujizuia?

Kilichonifanya nijione naingia katika hatari ni kwamba, juzi kushinda jana nilikwenda guest na msichana fulani nilikutana nae juu juu tu, tukafanya mapenzi na tulipomaliza wakati tunatoka kuna jitu la miraba minne lilikuwa likituangalia sana na yule msichana akashtuka sana.

Baadae nilipomuuliza akasema yule jamaa anafanya kazi na mume wake ni FFU kitengo cha doria.

Hakika nikaona hiki ni kifo cha wazi sasa na nimefikia pabaya, haya mambo sipangi ila imekuwa kama ulevi na siwezi kuacha.

Naombeni ushauri wa kunijenga wadau